Tuesday, August 30, 2011

Aisha Mbaga

MbagaMambo vupi mpenzi msomaji wa safu hii ya mahaba? natumai kwa uwezo wa Mungu amekujaalia pumzi na umzima wa afya hapo ulipo unaungana nami katika mambo ya mahaba.
kama ilivyo ada ya mapenzi kuwa ni makubaliano kati ya wawili basihakuna haja ya kulazimishana katika kufanya mapenzi, hii ndiyo mada yetu ya leo.
Ukipendana na mtu kwa dhati, mtaheshimiana, hutafanya kitu chochote cha kumwuudhi au kumwuumiza, hutamlazimisha mwenzio kufanya kitu ambacho hapendi au hataki na wakati wote utataka kumfurahisha.
Kitu kimojawapo ambacho kitakutokea wakati unakua ni kuwa na mpenzi aliyekuingia moyoni au kupata mapenzi mazito.
Kumpenda mtu kunaweza kuwa kuzuri. Lakini mara nyingine kunaweza kukuchanganya akili hususan yanapojitokeza mambo ya kufanya mapenzi.
Wapo ambao wanafurahia mapenzi kwa kuwa wanapendana na wenzi wao lakini pia wapo wanaotamani kufa ama kujuta kuzaliwa kwa kuwana wapenzi ambao hawajatulia.
Ili kuepukana na majonzi hakikisha kuwa unayempenda naye anakupenda kisha hana papara ya ngono.
lama kwli anakupenda atakuvumilia nawe hakikisha kuwa unakuwa na msimamo wa kutofanya ngono hadi uwe tayari. ZIngatia mambo yafuatayo ikimpata mpenzi ili kuhakikisha kuwa unamsoma na kuupa moyo wako nafasi ya kufanya maamuzi.
LAZIMA MFANYE NGONOUkiwa na mpenzi unayempenda kwa dhati haina maana kwamba ni lazima mfanye nae mapenzi. Kitendo cha kufanya mapenzi kinatakiwa kiheshimiwe na kipewe hadhi yake kwa hivyo usikiendee kwa papara!
SUBIRI mpaka ukiwa tayari kimaumbile na kimawazo. Unaweza kuanza kufanya mapenzi ukiwa katika mapenzi ya dhati na ambayo unayaona yanaweza kumudu vishindo vyote.
USIKUBALI KUDANGANYWAUkiangalia filamu karibu zote zinazooneshwa siku hizi au ukizungumza na marafiki zako unafikiria kwamba kila mtu anafanya mapenzi wakati wote. Hii sio kweli kabisa! Watu wengi wanasubiri mpaka watakapokuwa watu wazima au wakishaolewa au kuoa.
EPUKA UONGO KATIKA MAPENZIUwapo utaweza kuwa mkweli kwa huyo unayemtarajia, ni wazi kuwa mnaweza kuelewana na ni rahisi sana kugundua tabua zake kwa kuwa wakati wote utakuwa mwazi kwake naye atajutahidu kuwa wazi na ukiona mpenzi wako ni mwongo basi hakufai tafuta njia ya kumfanya awe mkweli ama heri kukaa na kumtafuta mkweli kwani baadae unaweza kujutia mahusiano yako.
Unaweza kumpenda mpenzi wako na kuamua kutofanya naye mapenzi. Kama mpenzi wako anakupenda kwa dhati basi ataheshimu uamuzi wako na atakuwa mkweli kwako ikiwa ni pamoja na kukutunzia heshma yako.
pamoja na mila na desturi za Waafrika, mwanamke ameonekana kwa yeye ndiye anayelazimishwa kufanya ngono wakati hawako tayari, Hata wavulana wanalazimishwa kufanya mapenzi na wapenzi wao au hata marafiki zao. Sio vizuri kwa marafiki kuwashawishi wasichana au wavulana kufanya mapenzi wakati wao hawako tayari.
basi kwa leo tuoshie hapa ila usisahau kujiunga nami wiki ijayo,kwa waswaki na maoni wasiliana namoi kwa barua pepe yangu
Na Aisha Mbaga
Mambo vipi msomaji wangu wa safu ya Mahaba? Natumai kwa uwezo wa Mwenyezii Mungu umzima wa afya na waendelea vyema katika maandalizi ya mwanzo wa wiki.
natumai wiki iliyopita tuliangalia jinsi ya maandalizi ya wakati wa tendo la kujamiaana.
ninaimani nimeeleweka kwa wale waelewa. nawashukuru walionipigia simu kunipongeza na kunitaka ushauri.
Dada yangu salha wa Arusha ananiuliza jinsi ya kumlea Mwanaume, usijali, Salha kwani mwanaume mbele ya mwanamke ni sawa na mtoto mdopgo, waweza mliza upendavyo ila unachotakiwa ni kuwa mbunifu.
Leo tutazingumzia mambo muhimu katika kufikisha hisia zako. wapo baadhi ya watu hawawezi kumweleza mwanaume ukweli kuwa anampenda na matokeo anabaki akiumia bila kujua la kufanya. kwa upende wangu mimi sioni aibu endapo najikuta nipo penzini nakiwa mwazi.
jambo la kufanya kwa mwanaume umpendaye naye hajui kuwa unampenda, kwanza mwambie kama uwezo wa kufanya hivyo unao. wapo wanawake jasiri kwa kuweka mambo bayana na kujikuta wengine wanafanikiwa kutatua matatizo yao. baadhi ya watu wanaamini kuwa, kumweleza mwanaume ukweli kuwa unampenda ni utamaduni wa wazungu, mimi naamini kuwa katika hisia hakuna mzungu wala mwafrika.
Endpo huwezi kuweka mambo bayana tumia nwiki wako kuhakikisha kuwa unamteka mwanaume huyo kwa kumtega kwa kutumia njia tano muhimu
njia ya kwanza kuweza kumtega mwanaume ni mavazi.
unaweza kumtega mwanaume unayempenda kw akuimia mavazi, jaribu kuvaa vivazi vya kumvutia na kumfanya atahamaki kwa kukuwaza kila amapo kumbuka kivazi chako.
fanua jitikada za kujipitisha pitisha kila mara kwake huku ukiwa na vizawadi ambavyo vitamfanya awe rafuki yako na kumweleza wazi kuwa unapenda kuwa karibu naye hatakama hataki kuwa mpenzi wako.
jia ya pili, pendelea kutoka naye kila wakati ikiwa ni moja ya njia ya kumhamasisha na utokapo kuwa unamshangaza kwa kumpa zawadi ama kumwandalia chakila maakum ambacho unauhakika atakipenda na kitamvutia.
tumia sauti yako katika mazungumzo ili aweze kuvutika nayo kwani katika mahusiano, sauti inaweza kuchukua nafasi kumshawishi mwanaume na kujikuta akiiwaza na kuingia mtegoni.
pia hakikisha kuwa macho yako yanazungumza kwa kumtazama na kila ayaonapo ataona vimrlea vya mapenzi ndani ya mboni ya jicho lako na kujikuta kuwa anasogea karibu na wakati mwingine anaweza kukushangaza kwa kukuambia kuwa anakupenda japo hakuwa tayari kuwa na wewe.
wakati mwingine si lazima mwanaume aanza kupenda hata wanawake wanapenda na wananafasi ya kuonyesha mapenzi yao na kuhangaika hadi kufanikisha penzi lake kw ayule ampendae.
kwa leo tuishie hapo na usikose kuungana nami wiki ijayo. Alamsiki
kwa maoni na ushauri wasiliana nami kwa simu 0755690690.

Nawatakia watoto wenzngu wote maisha mema. na wale waishio katika mazingira magumu, mungu awasaidie waweze kuodokana na maisha hayo. nawaasa wamuombe mungu atawasaidia. wafadhili na matajiri wajitokeze kuwalea watoto hao ili wasijiingize katika makundi yasiyofaa.

Na Aisha Mbaga


UCHUMI wa MALAWI

UCHUMI-MALAWI:Kuwa ''Mwanafunzi Bora'' Kunaweza Kuwa Kubaya Kwako Pilirani Semu-Banda BLANTYRE, Aprili 17 (IPS) - Miaka mitano baada ya njaa ambapo zaidi ya watu 1,000 nchini Malawi walifariki dunia na wengine milioni 8 kati ya milioni 12 nchini humo walikabiliwa na njaa, kumbukumbu inayouma ya ushauri wa sera mbovu bado inaendelea. Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF) na Benki ya Dunia zililaumiwa kutokana na janga hilo ambalo liliipiga Malawi wakati wa njaa ya mwaka 2002. Shirika la kimataifa la kupigania haki za binadamu la Action Aid, kwa mfano, lilionyesha katika taarifa ya mwezi Oktoba 2002 kwamba IMF imeitaka serikali ya Malawi kuuza akiba ya nafaka kulipia deni lililokopwa na chombo kilichosajiliwa kisheria cha Wakala wa Hifadhi ya Chakula ya Taifa (NFRA). Ripoti hiyo iliyojulikana kama, ‘‘State of disaster: Causes, consequences and policy lessons from Malawi'', pia ilitaja Benki ya Dunia. Action Aid iliilaumu Benki ya Dunia kutokana na ‘‘kushinikiza'' Malawi kuuza mahindi kwa Kenya kulipia deni ambalo nchi hiyo ilikuwa ikidaiwa na Benki hiyo. Halafu Waziri Bakili Muluzi pia alitangaza wazi wazi kwamba Benki hiyo imekuwa ikishawishi serikali kuhifadhi fedha za kigeni kuliko nafaka. Nafaka, Benki hiyo ilisema, zinaweza kupoteza thamani. Hata hivyo, IMF na Benki ya Dunia zilikanusha shutuma hizo kwa kusema kwamba ‘‘zilikuwa washauri tu'' kwa serikali juu ya hifadhi yake ya nafaka. Walisema kwamba sababu za uhaba wa chakula nchini Malawi zilikuwa ngumu ikiwa ni pamoja na serikali kukaa kimya kutoa onyo la haraka, kupotosha habari katika masoko ya ndani na usimamiaji mbovu wa hifadhi ya chakula. Kufuatia shutuma hizo na kujibu shutuma hizo, mahusiano kati ya mashirika ya wafadhili na serikali yaliathirika. Hii ilisababisha kuchelewa kwa wafadhili kuchukua hatua wakati wa mgogoro wa chakula. Malawi imekuwa ikitegemea zaidi wafadhili kwa miongo minne. Fedha za wafadhili ambazo imeshazipata zinakaribia asilimia 40 ya bajeti ya taifa. Nchi hiyo imeshindwa kung’ata mkono ambao unailisha. Hivyo, pamoja na madai hayo ya sababu za mgogoro wa chakula, serikali ilikamilisha mageuzi ya kiuchumi katika kuzingatia masharti yaliyowekwa na Benki hiyo na IMF. Ikiwa kama zawadi, taasisi hizo zilifutia Malawi madeni yake mengi ya nje yanayofikia dola bilioni 2.97 Septemba 2006. Kumbukumbu za njaa hiyo na sababu yake bado zinaendelea kuwepo. Baadhi ya Wamalawi wanataka nchi hiyo kujinasua kutoka kwenye mtego wa taasisi hizo. Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo ya Jamii ya Umoja wa Mataifa, Thandika Mkandawire, ambaye yeye mwenyewe ni raia wa Malawi, ni mmoja wa watu ambao anahofia mahusiano ya nchi hiyo na nchi wafadhili na taasisi za fedha za kimataifa. Anasema pamoja na Malawi kubatizwa jina la ‘‘mwanafunzi bora'' wa Benki hiyo na IMF kati ya mwaka 1980 na 1990, nchi hiyo inasimama kama mshtaka wa mahusiano ya misaada katika miongo mitatu iliyopita. Kati ya mwaka 1979 na 1999 Malawi ilichukua nafasi miongoni mwa kile IMF ilikipatia sifa ya ‘‘mtumiaji wa muda mrefu mno'' wa vifaa vyake. Taifa hilo lilikuwa na programu sita na IMF. Miaka 17 kati ya miaka 20 Malawi ilikuwa chini ya programu moja ya IMF hadi nyingine. ‘‘Katika nyaraka za IMF na Benki ya Dunia zilizokuwa zikifanyia tathmini matokeo ya sera za uchumi wa Afrika kati ya mwaka 1981 na 1998, Malawi iko juu zaidi katika orodha ya ‘warekebishaji bora' huku ikiwa imejitokeza mara saba, ikifuatiwa na Uganda na Kenya zikiwa za tano,'' anasema Mkandawire. Pamoja na ‘‘sifa hizo'', pato la taifa la Malawi lilishuka kutoka dola za Kimarekani 156 mwaka 1980 hadi dola 143 mwaka 1990. Hata ilipofika mwaka 2003 Malawi ilikuwa bado haijafikia kiwango cha pato la taifa cha mwaka 1979, kulingana na takwimu za Benki ya Dunia. Ripoti ya umaskini na kukosekana kwa utulivu iliyotolewa mwaka jana na serikali na Benki ya Dunia inaonyesha kwamba kumekuwepo na mafanikio madogo mno katika kupunguza umaskini na kukosekana kwa usawa. Mchanganyiko wa ushauri mbovu wa kisera na utawala wa kimabavu umezalisha miongo miwili iliyopotea kwa Malawi, anasema Mkandawire. Hakupendezewa na kukubali makosa kwa taasisi hizo au Mikakati ya Benki hiyo ya Kupunguza Umaskini. Ushauri wao umesababisha kuanguka kwa uwekezaji wa umma katika mtaji wa kimaumbile na kibinadamu, anasema. ‘‘Jambo ambalo hawaonekani kulitambua ni kwamba ongezeko la makosa limesababisha uchumi ambao haujarekebishwa vizuri na kushikiliwa katika mtego wa ukuaji mdogo,'' anasema Mkandawire. Mkandawire ana wasiwasi zaidi na jinsi ya kuingiliwa na nguvu za nje kunavyosababisha mataifa ya Afrika kupoteza uhuru wake. Mwaka 2002 IMF ilisitisha misaada yake ya kiuchumi kutokana na kile ambacho imekiita usimamizi mbovu wa uchumi chini ya rais wa zamani Muluzi. IMF ilirejesha programu yake baada ya utawala wa Bingu wa Mutharika, ambaye aliingia madarakani Mei mwaka 2004, kukubali kutekeleza sera zinazosimamiwa. Kwa njia hii rikodi zinazoeleweka za kutekeleza sera ziliundwa ili kuwarejesha wafadhili. Utekelezaji wa sera kwa mwaka wa kwanza ulishuhudia IMF na Benki kuizawadia Malawi kufuta asilimia 90 ya madeni yake ya kigeni. Msamaha wa madeni ulitafsiriwa kwamba Malawi ingeokoa dola za Kimarekani milioni 100 kama akiba ya kununulia bidhaa zake kutoka nje kwa mwaka kwani nchi hiyo iliendelea kuwa na mtaji ambao ungetakiwa kutumika katika kulipia madeni. Mkuu wa sera katika Action Aid Malawi, Collins Magalasi, pia hajaridhishwa na tabia ya mashirika wahisani. Anatoa mwito kwa nchi mfadhili wakuu wa Malawi, serikali ya Uingereza, kuongeza msaada wake wa kifedha ambao katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ulifikia wastani wa pauni milioni 54.1 kwa mwaka, ambapo ni asilimia 0.0009253 tu ya pato la ndani la mwaka la Uingereza. Magalasi analaumu kuwa Wamalawi 70,000 wanafariki dunia kila mwaka kutokana na magonjwa yasiyozuilika. Kipato cha watu wote kikichanganywa hakilingani na ruzuku za kilimo ambayo Umoja wa Ulaya unatumia kwa wakulima wake. Wakati akielezea kuridhishwa kwake na misaada ya wafadhili ambayo nchi hiyo inapokea, Mutharika ametoa pia mwito wa ‘‘sera zinazobuniwa ndani ambazo zinapaswa kuungwa mkono na washirika wengine''. Katika mwaka wa fedha 2005/2006 serikali ilianza kutekeleza sera iliyoandaliwa ndani ya nchi iliyojulikana kama Mkakati wa Kukuza Uchumi na Maendeleo wa Malawi (MGDS), ambao utaendeshwa kwa kipindi cha miaka mitano. Mutharika anaona mkakati huo mpya kama chombo cha kuhamisha vipaumbele kwani ulibuniwa na Wamalawi. Wakati huo huo, unafanya kazi ya kurejesha nidhamu katika masuala ya fedha. Wafadhili wameunga mkono sera hiyo, kwa kukubali kuruhusu nafasi kwa sera zinazobuniwa na Wamalawi; na watu wa kawaida badala ya zile zinazobuniwa na wanauchumi na kuzimiliki. Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Haki ya Uchumi wa Malawi (Mejn), Andrew Kumbatira, anakubaliana kwamba MGDS ni sera iliyobuniwa ndani ya nchi ambapo mawazo ya ndani yamepewa nafasi kubwa mno. Anakubali kwamba ‘‘kuna sera zinazofanana na hizo katika mataifa mengine yanayoendela. Hii inaonyesha kwamba sera bado inaongozwa na wafadhili. Lakini jambo zuri kuhusu sera hii mpya ni kwamba mikutano ya ndani ya mashauriano ilikuwa mingi''.

No comments:

Post a Comment