Tuesday, August 30, 2011


SI MAKOSA YETU NI MAKOSA YENU KUTUTENGANISHA.

Hayo ni maneno yaliyozungumzwa na wanandugu wa baba na mama mmoja. Inakuwa vigumu na anaendelea kuniwia vigumu kuvumilia kisa cha dada na kaka kuishi pamoja kama mke na mume na kuzaa watoto.
Ni familia moja ya kitajiri ambayo wazazi wao walitengana na kugawna watoto.
baba alichukua mtoto wa kiume na mama akamchukua binti yake.
Katika makuzi ya watoto hao hawawahi kujuana kuwa ni ndugu kutokana na kila mmoja wao kulelewa na mzazi mmoja na kufichwa juu ya mwenzie. usemi wa hakuna siri duniani unasimama pale wanandugu hao wanapokutana na damu zao kuvutana kiasi cha kila mmoja kuwa na hisia za kimapenzi kwa mwenzie.
Hawakuficha hisia zao, kila mmoja aliweka bayana ajisikiavyo kwa mwenziwake. mwisho wa yote waliamua kuishi kama mtu na mpenziwake na wakazaa watoto wanne.
mtihani unakuja pale ambapo wanagundua kuwa ni damu moja na jamii kuwataka watengane. hilo limekuwa gumu na kwao halitowezekana kwani kwa sasa wanafanya taratibu za kufunga ndoa. wao wenyewe wanasema wanapendana na hawawezi kuachana.
kama ni makosa wao kukutana na kuwa wapenzi ni ya wazazi wao na si kosa lao kwa ni endapo wazazi wao wangewakutanisha mapema wasinge fikia hapo walipo kwa sasa. wazazi wa watoto hao walijengeana chuki na kila mmoja kummiliki mtoto mmoja kama mali yeke na hakuna ambaye alitaka kumpeleka mtoto aliye naye kwa mzazi ambaye yuko mbali naye.
matatizo hayo hutokea mara nyingi pale familia zinapokorogana.
lamsingi ni kwamba wanandoa wanaposhindwana , wasiwatenganishe watoto ili kukwepa majanga kama hayo ya mtu na dadake wa kuzaliwa tena baba na mama mmoja wanaishi kama mke na mume na tayari wanawatoto na wameapa kila mmoja wao kuwa hawataachana labda kifo kiwatenganishe kama maandiko matakatifu yasemavyo.
Ndivyo Dunia ilivyo hivyoo.

No comments:

Post a Comment