Tuesday, August 30, 2011

Utalii; Kitovu cha Maendeleo
Visiwa hivi vya marashi ya Karafuu, ni maarufu kwa fukwe zake maridadi, matumbawe
na mji wenyewe wa kihistoria; Mji Mkongwe. Kwa maana hiyo, utalii ni sekta muhimu
katika uchumi wa Zanzibar na huchangia asilimia 26 kwa pato la taifa na uchangiaji huo
unatarajiwa kukua kwa kati ya asilimia 5 na 10 kwa mwaka.
Manispaa ya Zanzibar ni injini muhimu zaidi katika sekta ya utalii. Mji huu ndio lango
kubwa la watalii, achilia mbali wenyewe kuwa kivutio. Kabla ya watalii kwenda pwani ya
mashariki, kwa kawaida hukaa kwa muda katika Mji Mkongwe kufurahia mandhari yake
(tazama ramani 2.1)
Moja Ya Sehemu Za Ufukwe Kisiwani Zanzibar
Mitaa myembamba ya mji huu, hali ya hewa iliyotulia, majengo ya kale, milangu
inayopendeza iliyochongwa kwa mtindo wa aina yake ya kuviringwa, maegesho na
fukwe ndivyo vitu vinavyowavutia zaidi watalii hapa. Mji huu Mkongwe unazo hoteli
nyingi, migahawa na maduka kwa watalii ambayo pia hutoa ajira kwa watu kutoka
Unguja, Pemba na hata Tanzania Bara.
Idadi ya hoteli zenye hadhi za kulaza wageni imeongezeka kwa kiasi kikubwa katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita. Hata hivyo, hakuna uhakika wa hasa ni hoteli ngapi
zinazolaza watalii mjini hapa. Makadirio mengi yanaonyesha kwamba kuna vyumba
karibu 20,000 vya kulala kote kisiwani, na takriban asilimia 50 ya hizo, iko mjini.
Kamisheni ya Utalii ilirekodi ongezeko la asilimia 25 ya vyumba vinavyokodishwa kwa
watalii tangu mwaka 1987 hadi 1997. Jumla ya watalii walirekodiwa kuingia uwanja wa
ndege na kwenye bandari mbalimbali katika kipindi hicho, ni 587,640.
Sera ya Utalii Zanzibar imekuwa ikiegemea katika falsafa ya ubora wa hali ya juu na ujazo
mdogo wa watalii, mambo yanayoleta mapato makubwa kiuchumi kutoka kwenye sekta
hiyo, kwa ajili ya watu ambao ni wengi kisiwani, huku kukiwa na rasilimali chache.
Mwaka 1997, zaidi ya watalii 86,000 walitembelea Zanzibar wakati mwaka 1998, zaidi ya
watalii 100,000 walitarajiwa (tazama chati juu ya idadi ya watalii).
Japokuwa majengo ya kale hayapo Mji Mkongwe pekee, umaarufu wake unatokana
zaidi na kuwa mji wa kihistoria ambao pia ni makazi, ukiwa na majengo yenye
kupendeza, milango ya aina yake iliyoviringwa juu na kurembwa vilivyo, mitaa
myembamba ambayo watalii huishangaa na kufurahia sambamba na maisha ya jumla ya
Zanzibar.
Kivutio kingine kwa watalii ni rasilimali za bahari zilizopo. Ni kweli kwamba fukwe
zilizoko ndani ya Manispaa ya Zanzibar ni chache, visiwa vilivyo mbele ya mji, vina
matumbawe ya kupendeza ambayo ni maridhawa kwa ajili ya kuzamia na hata kupiga
mbizi. Uvuvi Kisiwani Zanzibar na Tabia Zake
Mazingira ya uvuvi Zanzibar ni ya kupendeza na inakadiriwa kwamba mwaka 1997, kiasi
cha watu 12,000 walirekodiwa kama wavuvi na vyombo vya uvuvi vilivyokuwepo wakati
huo ni 2,700.
Idadi kubwa ya watu (kwa mfano mwaka 1990, watu 6,000 kwa Pemba na Unguja),
hufanya kazi hutoa huduma katika sekta hii na huduma zihusianazo. Asilimia 22 ya
bajeti za kaya hutumika kununua samaki ambao ni chanzo kikubwa cha protini
Zanzibar, hasa kwa wale wenye kipato kidogo.
Manispaa ya Zanzibar ina vituo tisa vya kuvulia samaki ambavyo ni Malindi,
Malindi/jetty, Kizingo, Forodhani, Maruhubi, Kilimani, Mtoni, Mazizini na Bububu
(tazama ramani 2.3). Wastani wa samaki wanaovuliwa baharini katika maeneo ya Unguja
na kuletwa Manispaa ya Zanzibar ni takriban tani 2,273 kwa mwaka. Idadi ya samaki
wanaovuliwa kote Zanzibar ni kati ya tani 10,000 hadi 20,000 kwa mwaka na hii ni kwa
mujibu wa utafiti uliofanywa na Kamisheni ya Ardhi na Mazingira.
Wavuvi wenyeji hutumia karibu asilimia 96 ya samaki wanaowavua kwa soko la hapa
hapa, na wanaouzwa nje ni asilimia 4 tu. Kwa sasa, Manispaa ya Zanzibar ina kampuni
moja tu ya uvuvi iliyosajiliwa, yenyewe ikijulikana kama ZAFFICO. Ina waajiriwa wa
kudumu 60.
Wavuvi wengi wana vifaa duni na ndio sababu hasa ya uchache wa samaki wanaovuliwa.
Japokuwa takwimu zilizopo na za kuaminika hazitoshi, kuna vyanzo vinavyoonyesha
kwamba jumla ya idadi ya samaki waliopo kwenye maeneo haya, inapungua.

Uvuvi katika Manispaa ya Zanzibar unahusisha wale wavuvi wa asili na wengine ambao
wamekuja kufanya hivyo baadaye kwa sababu za kibiashara. Hawa wa asili,
wanaoonekana kama wasanii, hutumia vyombo vya uvuvi vya kijadi na mbinu za
kizamani, tofauti na wale wa kisasa ambao hutumia boti au vifaa vyenye injini.
Hawa wa asili huweza pia kutumia mishipi au fito na huweza kupata samaki wa
miambani na wa maji wazi kama kingfish na tuna. Wale wavuaji wa kibiashara zaidi
hupata samaki wa jamii ya bangala na wengine wadogo wadogo.
Samaki walioletwa Manispaa ya Zanzibar na kiasi chake kwa tani, thamani ikiwa katika
milioni za shilingiUchimbaji Zanzibar ni wa aina ndogo, ukilenga zaidi katika mchanga, mawe,
changarawe, chokaa na mchanga wa fukweni. Maeneo haya ya machimbo ni ya saizi
ndogo na ya kati na yamesambaa maeneo mbalimbali kisiwani.
Maeneo rasmi ya machimbo ni machache nje ya mipaka mipya ya mji, mmoja ukiwa ni
wa mchanga, katika eneo lenye ukubwa wa hekta mbili kwenye Wilaya ya Kaskazini B
na mengine mawili ya uchimbaji mawe na eneo moja la uchimbaji chokaa Wilaya ya
Magharibi. Mjini hakuna eneo rasmi la machimbo lakini hayo yaliyopo nje, hutumika
kwa ajili ya mji huu kwani inakadiriwa kwamba asilimia 90 ya yanayochimbwa huletwa
mjini.
Bidhaa hizo hutumika zaidi kwa ajili ya shughuli za ujenzi. Kuna maeneo mengine mengi
yasiyo rasmi, hasa kwa ajili ya kuchimba mchanga na ambayo hutumiwa ndani ya
manispaa, hasa katika maeneo jirani. Mchanga unachimbwa pia kinyume cha sheria
kwenye maeneo kama Mpiga Duri, Daraja Bovu, Amani, Welezo na Mpendae na
maeneo mengine kwenye kingo za mito. Ni vigumu kudhibiti hali hii kwani wachimbaji
hufanya kazi hiyo usiku. Jasi na udongo huchimbwa Mtoni, Chumbuni na Magogoni.
Ni kawaida kuona ngamia au ng’ombe dume wakibeba nyenzo hiyo vya ujenzi. Maeneo
yaliyoathirika zaidi ni Amaani, Magogoni na Maruhubi. Vitendo hivyo visivyo rasmi na
visivyoratibiwa katika Manispaa ya Zanzibar, vilisababisha mjadala mkali kwenye Baraza
la Wawakilishi kutokana na mmomonyoko wa ardhi. Japokuwa ilikubaliwa wizara husika
ichukue hatua, hali imebaki kuwa hivyo hivyo
Kilimo kimekuwa daima na umuhimu mkubwa kwa uchumi wa Zanzibar. Siku
zilizopita, uchumi ulitegemea kwa kiasi kikubwa mauzo ya karafuu na nazi nje ya nchi.
Hata hivyo, kupungua kwa bei kwenye masoko, kunaathiri kwa kiasi kikubwa mazao
hayo.
Katika Manispaa ya Zanzibar, kilimo kina mguso kidogo katika maendeleo ya mji.
Kilimo cha mjini ni kidogo, kama bustani tu na wajibu wa mji huu katika kilimo, ni kwa
vile tu mji huu ni soko kubwa kwa bidhaa za kilimo. Katika Mji Mkongwe hapafanyiki
kilimo, bali kinafanyika maeneo ya Ng’ambo lakini nako, kilimo kinashuka.
Maeneo ambayo kilimo kinafanyika zaidi ni Kilimani, Maruhubi, Saateni, Migombani -
Kaburi Kikombe, Kwaalinatu - Ziwani, Chumbuni, Mtoni, Kwahani na Sebleni, maeneo
yenye kiasi cha hekta 95. Mengi ya maeneo haya huzalisha chakula na mengine
yamegeuka kuwa mabwawa, hasa nyakati za mvua. Mpunga ndio zao kubwa linalolimwa
huko, likifuatiwa na ndizi na mboga kama vile spinachi, kabichi na nyinginezo. Katika
maeneo makavu kisiwani, viazi vitamu na mihogo hulimwa pia.
Maeneo haya yanatambuliwa rasmi na Wizara ya Kilimo, na wakazi hujitahidi kupanda,
japo miti michache ya matunda kwenye maeneo ya nyumba zao. Wengi wanaojihusisha
na kilimo cha mjini ni wanawake.
Mifugo kisiwani ipo pia, nayo ni kama ng’ombe, mbuzi, kuku, ngamia, bata na paka
ambao hupatikana maeneo ya Ng’ambo. Kuku na bata ndio wapo kwa wingi,
wakifuatiwa na ng’ombe na mbuzi. Maeneo ya Ng’ambo yenye mifugo mingi zaidi ni
Kiembe Samaki, Mwanakwerekwe, Mtoni, Bububu. Chukwani na Chumbuni.
Kwa sasa, mifugo katika kisiwa chote, huchangia asilimia 12 ya pato la taifa. Kuna
mipango ya kuboresha zaidi sekta hii ili kupunguza utapiamlo na pia kufikia mahitaji
halisi kwa wakazi wa mjini na sekta ya utalii. Kwa mujibu wa sensa ya mifugo ya mwaka
1993, kuna mifugo 73,000 katika visiwa vya Pemba na Unguja na kati ya hiyo, 13,000
ipo Wilaya za Mjini na Magharibi.
Katika maeneo ya kingo za mji, kwenye udongo wenye rutuba kwa ajili ya kilimo, ardhi
inagombewa kwa sababu mji nao unapanuka. Mashariki mwa mji, hasa maeneo
yaliyokuwa yakitumiwa kwa kilimo awali, sasa yanalazimika kuendelezwa kwa makazi.
Hali hii hupunguza maeneo ya uzalishaji chakula lakini pia husababisha mmonyoko wa
ardhi.
Kilimo kimekuwa daima na umuhimu mkubwa kwa uchumi wa Zanzibar. Siku zilizopita,
uchumi ulitegemea kwa kiasi kikubwa mauzo ya karafuu na nazi nje ya nchi. Hata hivyo,
kupungua kwa bei kwenye masoko, kunaathiri kwa kiasi kikubwa mazao hayo.
Katika Manispaa ya Zanzibar, kilimo kina mguso kidogo katika maendeleo ya mji.
Kilimo cha mjini ni kidogo, kama bustani tu na wajibu wa mji huu katika kilimo, ni kwa
vile tu mji huu ni soko kubwa kwa bidhaa za kilimo. Katika Mji Mkongwe hapafanyiki
kilimo, bali kinafanyika maeneo ya Ng’ambo lakini nako, kilimo kinashuka.
Maeneo ambayo kilimo kinafanyika zaidi ni Kilimani, Maruhubi, Saateni, Migombani -
Kaburi Kikombe, Kwaalinatu - Ziwani, Chumbuni, Mtoni, Kwahani na Sebleni, maeneo
yenye kiasi cha hekta 95. Mengi ya maeneo haya huzalisha chakula na mengine
yamegeuka kuwa mabwawa, hasa nyakati za mvua. Mpunga ndio zao kubwa linalolimwa
huko, likifuatiwa na ndizi na mboga kama vile spinachi, kabichi na nyinginezo. Katika
maeneo makavu kisiwani, viazi vitamu na mihogo hulimwa pia.
Maeneo haya yanatambuliwa rasmi na Wizara ya Kilimo, na wakazi hujitahidi kupanda,
japo miti michache ya matunda kwenye maeneo ya nyumba zao. Wengi wanaojihusisha
na kilimo cha mjini ni wanawake.
Mifugo kisiwani ipo pia, nayo ni kama ng’ombe, mbuzi, kuku, ngamia, bata na paka
ambao hupatikana maeneo ya Ng’ambo. Kuku na bata ndio wapo kwa wingi,
wakifuatiwa na ng’ombe na mbuzi. Maeneo ya Ng’ambo yenye mifugo mingi zaidi ni
Kiembe Samaki, Mwanakwerekwe, Mtoni, Bububu. Chukwani na Chumbuni.
Kwa sasa, mifugo katika kisiwa chote, huchangia asilimia 12 ya pato la taifa. Kuna
mipango ya kuboresha zaidi sekta hii ili kupunguza utapiamlo na pia kufikia mahitaji
halisi kwa wakazi wa mjini na sekta ya utalii. Kwa mujibu wa sensa ya mifugo ya mwaka
1993, kuna mifugo 73,000 katika visiwa vya Pemba na Unguja na kati ya hiyo, 13,000
ipo Wilaya za Mjini na Magharibi.
Katika maeneo ya kingo za mji, kwenye udongo wenye rutuba kwa ajili ya kilimo, ardhi
inagombewa kwa sababu mji nao unapanuka. Mashariki mwa mji, hasa maeneo
yaliyokuwa yakitumiwa kwa kilimo awali, sasa yanalazimika kuendelezwa kwa makazi.
Hali hii hupunguza maeneo ya uzalishaji chakula lakini pia husababisha mmonyoko wa
ardhi.

No comments:

Post a Comment