Tuesday, August 30, 2011

Leo nimeona niongelee hii issue nzima ya serikali kuanzisha kampeni kabambe ya kuwakamata madaktari na kufunga mahospitali yanayo jihusisha na UTOAJI MIMBA…
Ofcouse sheria ya Tanzania hairuhusu watu kuchoropoa mimba. Ila hivi Serikali imefikiria the end result ya hii kampeni yao?
Niliona kwenye news ya TBC1 last week jinsi serikali ilivyofunga vituo kadhaa vya marie stoppes nchini kwasababu ya kukutwa wanajihusisha na utoaji mimba.
Basi juzi nilikuwa kwenye maongezi na watu kama wa 4 juu ya hili swala na wote tulikubaliana kwamba ni matatizo makubwa zaidi yatakayotokana na hii kampenzi. MORE BAD THAN GOOD WILL COME OUT OF THIS.
Unajua hata miji kama Dubai wanasheria inayosema kwamba mwanaume na mwanamke ambao hawajaona hawaruhusiwi kuishi pamoja, ila watu bado wanaishi pamoja na serikali imeamua kufumbia jicho hilo swala kwasababu wameona kuna mambo ambao ni ya muhimu zaidi kwa wao kuyafanya Dubai than kufatili nani analala na nani ili wawafunge jela.
Sasa mdau unajua kwamba sasa hivi kutokana na kwamba serikali inawasaka madaktari wanaotoa watu mimba biashara ya utoaji mimba imekuwa ni biashara yenye kuingiza pesa sana?
Unajua kwamba sasa bei ya kutoa mimba imepanda kutoa elfu 50,000 mpaka 600,000 WTF?????
Na jana kuna dada kaniambia kuna rafiki yake alipata matatizo hayo akaongea na daktari wa moja kati hizi hospitali kubwa pale Mikocheni akaambiwa aje na DOLA 400 tena kwa mimba isiozidi 2 months akaambiwa he is risking his career ndio maana bei imepanda sana. WTF????? Hivi hiyo dola 400 si ni laki 6 hiyo??
Hivi kuna wanatanzania wangapi wanaweza kuafford laki 6 kwenda kutoa mimba?? Sana sana watoto wa shule,hivi serikali inataka tuanze kuzaliana kama wachina? Au watoto waache shule? Na Serikali imeshapiga hesabu ni watoto wangapi ambao ni unwanted watakuwa wanazaliwa kila mwaka kutoka nah ii kampeni yao?je wameweka mikakatati gani kudeal na hili swala na hili ongezeko la watu litakalotokana nah ii kampeni yao?? Au mkakati wao ni kuongeza kodi kwa wananchi ili waweze kusupport hawa watoto ambao wengi wao wataishiwa kutupwa majajalani au kwenye vituo vya kulelea watoto??
Kilichonifnaya nikaja kuongea hii kitu leo ni kwamba kuna mtoto wa form 2 wa shule moja mjini hapa,ambae alikuwa na ujauzito akaenda Marie Stoppes wakamwambia wanaogopa kumtoa mimba na kama anataka apelike laki nne kwasababu mimba yake ilikuwa kubwa , huyo msichana baada ya kuona hizo pesa hawezi kuzipata alichokifanya ni kwamba alikwenda pharmacy akanunua chloroquine akamix na dawa zingine za miti shamba ili mimba itoke, kesho yake alikutwa na mama yake akiwa amefariki yeye pamoja na kichanga chake tumboni.
Mimi naona serikali ina mambo ya maana zaidi ya kufatilia,badala ya kuweka kampeni kabambe za kupambana na rushwa na ujinga mwingine nchini humu wanafatilia mambo ya utoaji mimba sasa wanamkomesha nani? Hawaoni kama wanawakomesha wanawake wan chi hii na kuwatajirisha madaktari????
Nasikia kuna daktari mmoja kaanza kutolea watu mimba nyumbani kwake anachaji laki 320,000 unaambiwa ukienda pale unakuta foleni . yani hakosei wateja kama 10 kwa siku embu niambie kwa siku anatengeneza shingi ngapi kwa kuchoropoa watu mimba tu???
Hivi kweli ndani ya mienzi miwili tu bei za kutoa mimba zimepanda kutoka kati ya 30,000 na 50,000 mpaka kufikia laki 350,000 mpaka 600,000. its absurd.
Hatimae leo tumeshuhudia Japani ikiungana na timu kama engalnd, marekani na nyinginezo katika kuyaaga mashindano ya kombe la dunia
Pamoja na japani kutolewa katika mashindano hayo lakini mejitahidi mpaka tone la mwsho lakini bahati haikuwa yao.  katika huu mzunguko wa robo fainali ya kombe la dunia mechi hii ndio naiona kama imekuwa kinyumea na matarijio ya wengi kwani kila mtu aliamini kabisa kuwa japani ndio timu yenye kiwango kikubwa cha mpira kuliko Paraguay hivyo kumfanya kila mtu kusema kuwa Paraguay hawachuki raund lakiniimekuwa sivyo.
Japani ambayo hata katika viwango vya shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) inashika nafasi nzuri kabi huku ikiwa ni ni tuimu iliyokuwa ikiaminika kama ni miongoni mwa timu bora kabisa  kati ya timu zinazoshiriki michuano ya kombe la dunia lakini cha kushangaza leo inapelekwa pelekwa na Paraguay kama vile watoto wadogo yaani wamebanwa kila kona na kushindwa kuonesha manjonjo yeyote ambapo mpaka kipndi cha mapumziko paraguiay walikuwa wakiongoza kwa ball position.
Japani ambao waliingia kwa kasi ya ajabu katika kipindi cha pili lakini walishindwa kufikia lengo kutokana na kukuta bado Paraguay wamekaza kama mwanzo, pia Japan walipata fursa nyingi lakini washambuliaji wao walikuwa wataitiwa ile mbaya hivyo kuifanya timu nzima ya japa kuonekana hakuna ktu.
Japani ilifanya mabadliko ya kumtoa Yukiabe na kumuingiza Mukabere dakika ya 80 lakini haikusaidia kitu kwa Paraguay ilikaza mpaka dakika ya mwisho hivy kuongezewa dakika 30 tena za kupambana na katika daklika ya 15 katika zile dakika30 za za nyongea japani ilifanya mabadiliko mengine ya kumtoa Okubo na kumuingiza Tamada ili kuongeza mashambulizi lakini bado hali ilkuwa ngumu. Mpaka kufikia dakika ya mwisho mechi ilikuwa ni dro ikiwa hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzake hivyo kufanya refa awape penalt.
Dakika zote 30 zilikuwa ngumu kila upande kwa kutofungana na kasha kupeawa panalt tano tano. Katika panalt hizo hapo ndipo japani walipoona joto ya jiwe kwa kupigwa mikwaju yote mitano huku yenyewe ikikosa mkwaju mmoja nakuifanya ifungashe virgo na kurudi kwao japani huku wakiacha mashindano yakiendelea. Tusubiri mechi ya pili tuone nani ataibuka mshindi kati ya Hispania na Ureno ambae atakuja kucheza na Paraguay.

Kwanini wanaume husaliti penzi

kwanini wanaume husaliti penzi?

Na Aisha Mbaga

Mpenzi Msomaji wa safu hii, nakukaribisha tena tujumuike katika
Chumba cha Mahaba n ipate kukupa dondoo mbali mbvali juu ya
kuimarisha mepenzi na kujitambua zaidi juu ya swala zima la
mahaba.

Wiki iliyopita tulizungumzia juu ya matayarisho ya chumba cha
mahaba nikijumuisha na mbambo muhimu wakati wa
kujimwayamwaya na mpenzio, pia tulizungumzia juu ya matayarisho ya kitanda na jinsi ya usafi umalizapo mechi yako.

Leo mpenzi msomaja wa Tanzania Daima ndani ya Chumba cha
Mahaba tunazungumzia ni kwanini wanaume wengi hupenda kutoka nje ya ndoa zao ama kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.

Haimananishi kuwa mwanaume anapotoka nje ya mwenzi wake
amemchoka ama hamtaki, kinachotokea ni kwamba mwanaume
huvutwa na hali halisi ya maumbile ya mwanamke na kila wakati
hupenda kutafuta ladha fulani.

Kujua kuwa mwanaume huyo anamheshimu mpenzi wake wa
kudumu, atakuwa anafanya mapenzi hayo ya wizi kwa siri ili mpenzi wake ama mkewe asitambuwe kuwe anaibiwa.

Maranyingi wanawake huwa hawapendi kuwaona wenzi wao wakiwa na uhusiano wa mapenzi na mwanamke mwingine zaidi yake hivyo huwa na wivu mkubwa juu ya mpenziwake kufikia hatua ya kuwekeana uhasama na mwanamke atakayemgundua kuwa anamwibia penzi lake.

Ugomvi mwingi wa wanawake unakuja pale ambapo wanajikuta
wakishea mwanaume mmoja na kwa wkati mmoja huku kila mmoja akiwa na tumaini kuwa yuko pekeyake na mwanaume huyo kumtimizia kila mmoja haki yake kwa muda wake.

wanawake hao watakapogunguana, ajabu wanawekeana uhasama wao kwa wao bila kujua kuwa kati yao hakuna mwenye kosa kwani kila mmoja kwatakwa kwa muda wake na wakumlaumu ni yule mwanaume ndiye wangepaswa kukkaba awaeleze kinagaubaga.


Haimaanishi kwamba wanume ni malaya sana kuliko wanawake ndio maana hawatosheki matamanio yao, lahasha! hapa tunayazungumzia maumbile ya mwanaume kutokana
na kuvutika kihisia kwa mwanamke yeyote amwonaye kuwa na mvuto kwake.

Wakati mwingine wanawake tumekuwa kivutio kwa wanaume na
kuwaweka katika wakati mgumu huku tukielewa wazi kuwa
tunawatega. pamoja na kuwa tunakwenda na wakati, tunapaswa
kujua kuwa mwanamke hata avae juba, mwanaume akishamtamani lazima akidhi haja ya matamanio yake hata kama hatafanikiwa kwa mwanamke huyo, basi atatafuta mwanamke anayeendana na huyo.

hayo ndiyo maumbile ya mwanaume hivyo kwa mwanamke mwenye wivu unaweza ukajidhani labda humvutii mpenzi wako ama hupendezu kumbe wewe ni mzuri na unawavutia wanaume wengi kwani hakuna mwanake asiyekuwa na mvuto mbele ya mwanaume.

Ili kujua kuwa mwanaume anakupenda ila hufanya kosa kutokana
na maumbile yake, ni pale utakapomfumania akikusaliti, mwingine hukosa raha ama akajikuta akilia kujutia alichokifanya huku akiwa na hofu ya kuachwa.

Mwanaume mwingine huwa anakosa cha kuongea na
kupata kigugumizi cha ghafla ama kujikuta akikudanganya juu ya tukio hilo kuwa hakutegemea kama ingetokea, “Hakkujua kama angefanya”
kwa wanaume wengine hukujia juu ili kukupunguza jazba ama kukutisha ili usimuulize chochote na kisha baadae hukuomba msamaha. hizi zote ni baadhi ya tabia na maumbile ya wanaume.

Wapo ambao wanawatetea wanawake wanaofumaniwa nao kwa ajili ya kuwalinda isi wasidhuriwe na mwanamke muhusika kwani yawezekana lolote likatokea kati yao kisha mwanaume yule akaja kukuomba radhi na kukusihi kuwa hatorudia kosa hiyo imetokea kwa bahati mbaya akashindwa kujizuia.
Jinsi ya kujikinga na na kujaribu kumfanya mpenzi wako asiwe na
tamaa, mwache awe huru na mjengee mazingira ya kuona wivu na
kuhisi kuwa anaibiwa. kwa kufanya hiyo unaweza ukamweka
mwanaume wako katika mtihani na kumpa kazi kubwa ya
kukufuatilia hatua hadi hatua na kujikuta akikosa muda wa
kuwatizama wanawake wengine hivyo unakuwa umemwondolea tabia ya kuwatamani wanawake ovyo na kumpa kazi ya kukuchunga.

Haimaanishi kuwa mkawafanyae waume zenu hivyo, kwa kuwakomoa, jaribuni kuwafanyia ili kutengeneza penzi lenu. wapo ambao hawajali ukimwacha huru anashukuru na anakuwa naye anakuacha huru japo atakuwa anaumia kuwa huenda anaibiwa, atauficha wivu wake juu yako.

Hakuna mwanaume anayependa kuona kuwa anashea mwanamke na mwanaume mwenzake, huwa inawaweka katika wakati mgumu na niadhabu kubwa inayowaumiza japo wanakuwa jasiri tofauti na wanawake wanaoishia kulia na kujikondesha.

Hii ni tabia ya baadhi ya wanaume wengi kwani wivu wao upo
ndani na unawaumiza ndani kwa ndani lakini hawapendi
kuwaonyesha wanawake kuwa wanawivu juu yao.

mwanaume huwa atakuuliza tu kuwa yule ni nani na kwanini umesimama naye ama umekaa naye sehemu ya stare au faragha kama hiyo na hapo hapo atataka mchezo ili kuhakikisha kuwa hakuna aliyepita kwenye njia yake.

Nataka nikwambie jambo moja wewe mwanake mwenzangu ambaye unadhani kuwa labda mpenzio anakuona humzuri ndio maana anatoka nje na kukuacha ndani pekeyako.

kwanza usisuburikusifiwa kuwa wewe ni mzuri, cheo hicho jipe mwenyewe na anayekuona kuwa wewe ni mbaya usimkataze kufikiri hovyo kwani huo ni matazamo wa akili yake unavyodhani lakini amini wewe umzuri kuliko mtu mwingine yeyeto.

Pia usipende kumsema mwanamke mwenzio kuwa si mzuri, Mungu hajaumba binadamu mvbaya ila tabia ndio zinatofautiana kutokana na maumbile ya nafsi ya mtu mwenyewe upeo wa akili zetu.

Mwanaume wako anapotoka nje na ukajua, usimwambie chochote
zaidi ya kumsifia kuwa anachombo kipaya na kizuri kisha mpe
hongera na atakapo mambo fulani mpe, utakapomfanyia hivyo
utamnyima raha kwa kujutia alichokifanya na kuwaza kwanini
amekusaliti.

Japo kuwa ni maumbikle yamempelekea kufanya hivyo, atajilaumu na wakati mwingine atakuwa anataka kukufanyia jambio ili usahau ama umsamehe zaidi kosa lake la kusaliti penzi.
wakati mwingine wanawake wanapowafumania waume zao huanza kuropoka na kuwatukana, mmm! hatuendi hivyo dada yangu,
unapomfumania mwanaume wako msifie kwa urijali wake na kisha nyamaza kimya bila kumuuliza chochote.
kama ilivyo kawaida ukimya ni adhabu kwa wapendanao, unaponyamaza atataka kujua kuwa unafikiria nini kichwani kwako, atakosa raha kwa kujua kuwa huenda ukalipiza kisasi, atawaza
mengi juu ya ukimya wako na ukamfanyia hivyo kwa wiki moja, ukaenda kumpima uzito atakuwa amepungua.
yapo mambo mengine yanayopelekea mwanaume kusaliti penzi lake
kutokana na jinsi mpenzi wake anavyojiweka tofauti na kuwa maumbile ya mwanaume ni yamatamanio aonapo maumbile ya mwanamke.

Uchafu wa mwanamke nao unasababisha mwanaume kukimbilia anapoona kuwa panausafi na pengine kujikita huko kabisa japo wanadai kuwa gari huwa lazima ipate spea tairi, waweza ukajikuta
kuwa, mazingira uliyonayo yanakufanya wewe ndiye spea kuliko spea yenyewe.

Nataka kuwashauri wanawake wenzangu kuwa mwanamke mazingira.
Kujipakaa mafuta usoni ukang'aa lakini kule Ikulu iliyokufanya wewe ukaitwa binti na kuonekana mrembo huifanyii usafi kiasi cha kumkera kila anayeingia, jua utakuwa mtanashati wa uso na mavazi tu lakini kwimgineko mh! Hapafai.

Tambua kuwa hiyo Ikulu yako ndiyo inawasababisha hao wanaume mpaka wanapigana, yote ni kwasababu tu inamvuto na ndio maana waweza kumuona mwanaume anamng’ang’ania mwanamke ambaye hawaendani, eidha mwanaume ni mzuri sana kuliko mwanamke lakini hiyo si tija cha msingi ni umaridadi wa Ikuli.

Wahenga walisema si vyote ving'aavyo ni dhahabu ati, pia Uzuri wa mkakasi ndani kipande chamti na mimi nakwambia kuwa, kaa na marashi nawe unukie japo hujajipulizia lakini ukaapo na wenye
marashi nawe waweza onekana ni miongoni wao kumbe la.

Napenda wanawake tupunguze wivu na kwani unasababisha kujengeana majungi na wakati mwingine kudhiriana hata kwa kuuwana kisa ni wanaume ambao hata ufanye nini hakuna mwanaume wa pekeyako. Kasema hadija kopa kuwa Kamaunaweza
mtie kamba mumeo lakini ukitahamaki kachimba chini ninaye.

Basi mpenzi msomaji wa safu hii nisikumalizie uhondo kwa siku ya leo, nakushukuru kwa
kuungana nami. basi mpenzi msomaji tukutane wiki ijayo katika chumba hiki hiki cha mahaba na tutakuwa tunazungumzia ni kwanini wanaume huwahi kumaliza tendo la ndoa kabla ya wanawake.

Kwa ushauri au maoni wasiliana nami simu ya kiganjani namba 0755-690690 .
Na Aisha Mbaga

Mpenzi msomaji wa safu hii nakukaribisha tena uungane nami katika chumba changu hiki cha mahaba tuweze kujimwayamwaya na kujinafasi kwa raha zetu.Wiki uliyopita tulikuwa tukizungunzia udhaifu wa wanaume katika suaka zima la mapenzi na sababu zinazopelekea wao kuwa katika hali hiyo.tilibaini kuwa kwa upande mwingine wanakuwa na usongo wa kutimiza lengo hivyo wanapofika katika mchezo wakajikuta wameshindwa kuukwea mnazi, upande mwingine ni maumbile ya kibaiolojia na upande mwingine wanawale tunachangia kwa kutokuwa makini ama kujihusisha na mapenzi kwa wakati.leo nataka kuueleza jinsi wanawake walivyo wezi wa mabwana wa mashoga zao na jinsi wanavyoweza kusambaratisa penzi lililoota mizizi.
mwanamke anapotaka kukufanyia unyama kwa mpenzio hashindwi haswa pale unapokuwa umemweka karibu na mpenzio.kila mwanamke huwa na shoga na wengine hupenda kusema mambo ya kweli wanayoyapenda wapenzi wao na kumpa nafasi kubwa rafiki yake pale anapotaka kuporomosha penzi hilo.mwanamke anamitego mingi kwa mwanaume ikia i pamoja na kumpelekea zawadi ambazo mpenzi wake hampi.kumfanyia mambo ya mahaba ambayo hayapati kwa mpenzi wake na kisha kumtega kwa vivazi, na urembo wa asili. kina mavazi ambayo yamnamvutia mwanaume apende asipende, atatamani kuwa na wewe, mavazi haya si lazima yawe mini sket au top na pedo, waweza vaa hata baibui lakii kutokana na jinsi lilivyo likamvutia mwanaume na kujikuta anashindwa kujizuia na kuingia katika mtego wa mhaba mazito ambayo anadhani kuwa atayapatantoka kwako. kinachosababisha matatizo haya ni kutokana na kuaminiana kwa hali ya juu kati ya mashoga hawa na kuambiana siri zao za ndani juu ya wapenzi wao. ukweli ni kwamba, usipende kumweleza rafii yako mambo ya anayokufanyia mpenzio kwani unampa nafasi ya kuweza kumteka hususani anapojua kuwa mpenzio anaudhaifu gani. kama kunaulazima wa kuhadithiana juu ya wapenzi wenu, kuwa makini na wakati mwingine ni heri umwambia rafukiyo uongo ili kuweza kulinda penzi kwani kikulacho kinguoni kwako. wanawake wengi hawapendi kuona mwenzao kafanikiwa, ama kuona penzi la mtu likiwa imara, ni dhahiri kuwa wapo wanaochukia na kutafuta mbinu za kuliporomosha hata wakishindwa wao watatumia watu wa pembeni yenu bila ya wewe kujua kuwa shoga, rafikiyo mkubwa anakugeuka na kukuzunguka. waweza kusema sitaki kuwa na rafiki mwanamke kutokana na tabia za baadhi yao kuwa za unafiki na wivu kwa maendeleo ya mtu. kama ujuavyo mapenzi ni makubaliano kati ya watu wawili na yanaweza kuvunika muda wowote endapo wanaweza kushindana na kutofikia malengo. hilo si jambo la ajabu kwani ndio maana hata leo tunaweza kuona kwenye baadhi ya michezo ya tamthilia watu wakiamua kutalikiana ili kila mtu aishi kwa amani. ni mara chache sana waweza kumuona mwanake anasikitika kwa kuona penzi la mtu likiishia mitini hususan pale watu hawa wanapokuwa wachumba ama ndio kwanza wanaanza, achilia mbali waliooana na kuchokana. wanawake wengi wako makini kuhakikisha kuwa ndoa ya mtu fulani haifungwi na kufanikiwa kuvunja uchumba wa wawili hawa na wakati mwingine ndo kwanza maapenzi yanaanza lakini yataingiliwa na kidudu mtu na kuharibiwa. yote haya ni kutokana na mashoga na chanzo ni kupeana siri za wachumba wenu. tuweni makini na tuache kuaminiana kwani umwaminiye ndiye adui yako.

napenda kuwashukuru wasomaji wangu walionipigia simu na kunipongeza na pia kunipa ushauri, nakarubisha maoni yenu kwangu na nitayafanyia kazi bila kusita. pia napenda kumpa pole mama yangu ambaye aliniambia kuwa mumewe amekuwa kicheche kwa kutembea na watoto wadogo anaoweza kuwazaa bila kujali walipotoka na uzee walionao. napenda kumshauri mama huyu kutoka Tabata jijini Dar es Salaam kuwa asijali kuona mumee kamsaliti kwani hiyo ni kawaida ya wanaume wengi ila lamsingi namshauri amwombe wakapime afya zao kulingana na hali tuliyonayo.

kwa maoni na ushauri wasiliana nami kwa simu namba 0755-690690.

MAGOFU YA KILWA, KIVUTIO KWA WATALII

Magofu ya Kilwa ni kivutio kwa watalii.
Na Aisha Mbaga
Magofu ya kumbukumbu ya kihistoria, ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara yanayofanyiwa ukarabati yanatarajiwa kuongeza idadi ya wageni wanaotembelea eneo hilo kutoka ndani na nje ya nchi mara baada ya ukarabati kukamilika.
Mradi huo, unaendeshwa kwa pamoja na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, nchi ya Ufaransa, Japan na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utamaduni, Elimu na Sayansi (UNESCO).
Mradi huu wa maendeleo umepania kuinua utalii katika eneo hilo la lililopo kilomita 300 kusini mwa Dar es salaam.
Meneja mradi Bw.John Kimaro anasema kuwa kwa kutangaza eneo la kumbukumbu la magofu la Kilwa Kisiwani na Songo Mnara kutawaelimisha wengi ambao hawajapata taarifa hizo kwa undani.
Katika ukarabati huo maeneo yanayoshughulikiwa ni pamoja na jumba la kale la Gereza “Gereza Fort” lilojengwa na Wareno mwaka 1505 na kufanyiwa ukarabati upya na Waarabu mwaka 1807,ambalo limeshawekewa umeme “security light” unaotumia nishati ya jua “solar power”.
Magofu mengine yanayofanyiwa ukarabati katika eneo hilo lenye kilomita za mraba 2000 ni Husuni Kubwa yenye eneo la mita za mraba 3000 iliyojengwa karne ya 14 na Husuni Ndogo, Jumba la Makutani “ The Makutani Palace” Msikiti Mkubwa “The Small Mosque”, Makaburi ya Shirazi “The Shirazi Tombs”, na Songo Mnara.
Mhandisi katika mradi huo Bw. Pierre Blanchard anasema kuwa ukarabati unafanywa kwa kutumia vitu asilia vilivyotumika awali katika ujenzi wa magofu hayo kama vile chokaa, udongo mwekundu, na mchanga.
Anasema kuwa iwapo ukarabati utatumia vifaa vya kisasa kama, cement, dhana nzima ya utunzaji wa magofu hayo itapotea kwa sababu haviendani na uhifadhi wake.
Ukarabati unafanywa na vijana 15 wa Kitanzania ambao wamepata mafunzo kutoka kwa watalaam wa kujitolea wa shirika lisilo la serikali la nchini Ufaransa liitwalo Chantiers, Histoire and Architecture Medievales (CHAM) linalojishughulisha na elimu ya utunzaji wa kumbukumbu za kihistoria, kazi mbalimbali za kujitolea kwa vijana katika uhifadhi na mafunzo kazini kwa wale wasiokuwa na ujuzi.
Lengo la CHAM ni kuwawezesha vijana hao kupata uelewa kuhusu utunzaji wa magofu kwani baadhi yao awali walikuwa ni wavuvi au wakulima na wengine ni wasichana ambao hawajashiriki katika ujenzi kabisa.
Meneja mradi anasema kuwa kitajengwa pia kituo cha kutoa habari ili kutoa taarifa kwa wageni na watu wengine watakaokuwa na kiu ya kujua zaidi kuhusu eneo hilo la magofu lililotangazwa kuwa urithi wa Dunia mwaka 1981.
Hii ni moja kati ya hatua nyingi za kuitambulisha historia ya Kilwa kitaifa na kimataifa, na ni muhimu kwani tayari baadhi ya wadadisi wamesema kuna hatari ya vitu vilivyopo na historia yake kupotea kabisa barani Afrika iwapo havitatunzwa vizuri.
Kilwa kama ilivyo baadhi ya miji katika mwambao wa bahari ya Hindi ulikuwa ni kituo kikubwa cha biashara katika karne ya 13 na 14 hivyo kuvuta wafanyabiashara kutoka kona mbalimbali duniani.
Mji huo wa kusini ndio pekee uliokuwa na sarafu yake katika ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara (Sub Sahara Africa). Katika kipindi hicho biashara nyingi ilifanywa kwa kubadilishana vito (barter trade).
Inasemekana kuwa ingawa mambo mengi ya kale yanapatikana barani Afrika, Tanzania ikiwa moja ya nchi zenye kumbukumbu za kitamaduni za kale, wengi miongoni mwa wakazi wa Afrika hawaelewi chochote au wana uelewa kidogo mno kuhusu kumbukumbu hizo ambazo zinawahusu.
Kilwa ndiyo iliyokuwa na msikiti mkubwa katika karne ya 11 na 15 ambao hadi leo upo uliotumika wakati wa sherehe ukikusanya watu kutoka kona zote za mwambao hadi Mombasa na Sofala. Kulikuwa na misikiti 99 katika kipindi hicho ambayo baadhi magofu yake bado yapo.
Wapo wanaodai kuwa sehemu za ukanda wa kusini katika utalii zimesahaulika kabisa. Hata hivyo serikali na wahisani mbalimbali wanaboresha maeneo hayo yawe ya kuvutia zaidi kwa watalii na wageni mbalimbali mara wafikapo hapa nchini au wakiwa nje ya nchi wawe na shauku ya kufika na kujionea hazina za mambo ya kale zinazopatikana katika sehemu hizo.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa Bw. Bernad Itendele anasema kuwa wakazi wa eneo hilo wanafundishwa mambo mbalimbali ikiwamo namna ya kuwapokea watalii, kuwafunza utamaduni wao na kujifunza kutoka kwao bila woga.
Anasema kuwa wilaya hiyo imepata umaarufu katika utalii baada ya samaki aina ya Silicant zaidi ya miaka milioni 65 iliyopita kuvuliwa katika eneo hilo.
Pamoja na hayo, Mkurugenzi wa wilaya ya Kilwa, Bw. Muhando Harold Senyagwa anasema Daraja la Mkapa limeleta mabadiliko mengi, ikiwamo idadi ya wageni kuongezeka kila kukicha na upatikanaji wa usafiri wa uhakika.
Pamoja na juhudi nzuri zinazofanywa na serikali kwa kuwashirikisha wananchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo, ikiwamo utalii wa jamii, (community tourism) ili kuinua uchumi na hali za maisha, bado juhudi kubwa zaidi inahitajika ili kufikia viwango vinavyostahili hasa katika utalii ambao kila kukicha unakua kwa kasi ya ajabu.
Baadhi ya wakala wa watalii kutoka katika nchi za ulaya wana mtizamo kuwa bado huduma ya utalii inastahili kuboreshwa ili iendane na gharama zinazotozwa, ikiwa ni pamoja na wanaojishughulisha katika kazi za utalii kuwa na elimu kuhusu shughuli zao.
Takwimu za watalii waliofika nchini kati ya mwaka 1998-2002 zinaonyesha kuwa watalii kutoka Ulaya, wengi wanatoka katika nchi za Uingereza, nchi za Scandinavia, Ujerumani, Ufaransa, Italia, Holland, na Uswisi.
Inakisiwa kuwa ifikapo mwaka 2012 wageni watakaoitembelea Tanzania watafikia idadi ya watu zaidi ya 900,000 ambapo idadi hiyo kubwa ya wageni watakaofika itachangia kuongeza kipato katika sekta nyingine za uchumi.
Idadi ya wageni inaongezeka kwa sababu ya mambo mengi ikiwamo utunzaji wa vivutio vinavyopatikana hapa nchini unaofanywa na serikali na wananchi kwa ujumla hasa wale wanaozunguka maeneno ya utalii.
Aidha, Shirika la Hifadhi za Taifa la Tanzania (TANAPA) lilianzishwa mwaka 1959 pamoja na mambo mengine, kutunza hifadhi za Taifa ili zisivamiwe au kuharibiwa kwa namna yoyote kuwezesha wananchi na wageni mbalimbali kuzitembelea wakati wowote.
Kutokana na uhifadhi wa makini hasa wa maliasili Tanzania yenye eneo la kilometa za mraba 937,062 yaweza kujinadi kuwa ni moja kati ya nchi ambazo mtalii anaweza kufunga safari na kupumzika kwa kuangalia vivutio mbalimbali na kumbukumbu za zamani ambazo hazipatikani mahali pengine popote Duniani.
Katika kongamano la pili la Kimataifa la Afrika Kuhusu Nafasi ya Utalii Katika Kudumisha Amani lilofanyika hapa nchini Dr. Dawid De Villiers ambaye ni Katibu wa Shirika la Utalii la Dunia (WTO) aligusia kuwa bara la Afrika bado lina nafasi kubwa ya kufaidika na utalii, hata hivyo bado soko la sekta hiyo halijatumika ipasavyo kwa maendeleo katika jamii, bara la Afrika linawakilisha asilimia nne katika biashara ya dunia.
Alisema iko haja ya kuhakikisha picha mbaya inayolieleza bara la Afrika kama sehemu ya njaa, magonjwa na migogoro, ambapo wakati tatizo liko katika nchi moja au sehemu ndogo hali hiyo huchukuliwa iko katika bara lote.
Akizungumza katika kongamano hilo, Waziri Mkuu Mhe. Frederick Sumaye alisema kuwa tukio lolote la kigaidi linapotekea ndani au nje ya Afrika huleta picha mbaya hivyo kupunguza idadi ya watalii na wawekezaji wengine hivyo kudumuza uchumi. Takwimu zinaonyesha nchi 33 kati ya 48 masikini zipo katika bara la Afrika.
Ingawa bara la Afrika lina vivutio vingi ambavyo bado havijatumika kisawasawa kwa sababu ya matatizo mbalimbali, takwimu za WTO zinaonyesha kuwa sekta ya utalii inaingiza dola za Kimarekani (USD) trillioni 3.6 na kutoa ajira moja kati ya watu 12 duniani.
Hapa nchini, na nchi nyingine za Kiafrika utalii ni moja kati ya sekta zinazotegemewa katika kuingiza fedha za kigeni hivyo kuchangia kuondoa umaskini, ambao ni mkakati wa serikali ya Tanzania kwa kuwashirikisha wananchi kuondosha umasikini.
Hata hivyo, Raisi wa Shirikisho la Sekta Binafsi la Tanzania (TPSF) Elvis Musiba aliweka bayana kuwa sekta binafsi bado “imelala usingizi” kwa sababu ya ukubwa wa mtaji unaohitajika katika kuendesha sekta hiyo.
Aliongeza kuwa matumizi mabaya ya maliasili yataleta athari kwa utalii hivyo ni muhimu kwa wananchi katika sekta binafsi kuisadia serikali katika kupambana na wahalifu waharibifu wa maliasili ili kuleta utalii endelevu
Baadhi ya tafiti kuhusu maendeleo ya Afrika zinatilia shaka bara hilo kwamba haliko sambasamba na karne ya 21 ambapo kipato katika ukanda wa Sahara (Sub Sahara Afrika) kimekuwa kidogo kuliko ilivyokuwa mwishoni mwa miaka ya 1960.
Tafiti zinaonyesha kuwa kati ya Waafrika watano, mmoja yumo katika migogoro pamoja na hayo wale wenye ujuzi hukimbilia nchi za ng’ambo wakati idadi ya wakazi katika bara hilo imeongezeka mara mbili. Katika miaka 30 iliyopita.
Baadhi ya wadadisi wanasema kuwa ukianza na ujenzi wa mlango wa nyasi hakika utabadilika na kumalizia kwa ujenzi wa mlango wa chuma, hivyo mradi wa ukarabati wa magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara utaleta maendeleo kwa wananchi.
mwisho

kwanini tumekuwa wanyama